Tuesday, November 27, 2012

KILA MWENYE PUMZI NA AMSIFU MUNGU


WITO KWA WOTE WANAOPENDA KUMUIMBIA MUNGU.

Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Maranatha inayohudumu kwenye Huduma ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba wakiimba kwenye moja ya mikutano iliyo andaliwa na huduma .Picha Na Hisani ya Huduma.
                                                                       Waumini wa Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba wameaswa kujiunga na vikundi na bendi mbalimbali zinazomsifu mungu wakati wa ibada ndani ya huduma hii ili kuwezesha ibada kuwa ya msisimuko na shangwe mbele za mungu kwani mungu anapendezwa na sifa hasa kipindi mwanadamu anapeleka haja zake kwa mungu .
    Akizungumza katika moja wapo ya ibada za kawaida za jioni zinazofanyika mahali hapo alisema "Nijambo la aibu kuona kwaya zetu zinalegalega kuna wakati tunatakiwa tuwe na jeshi kubwa la kumsifu mungu ili kutikisa anga la shetani kwani katika sifa Mungu anawahi kushuka pia lazima iwepo praise and worship team (timu ya kusifu na kuabudu) itakayotuongoza kwenye kuimba tenzi na mapambio wakati wa ibada na mikutano hivyo nawasihii wote Mungu aliowapa karama hii kutumia nafasi hii vizuri"
       Aidha kiongozi huyo ameahidi kuboresha safu ya vyombo vya muziki vya huduma ikiwa na pamija na kuwapeleka baadhi ya wanakwaya na bendi kupata kozi ya muda mfupi itakayohusu ufundi wa mitambo na muziki ili kuondoa tatizo la kuharibika kwa vyombo mara kwa mara.Na kwa upande mwingine hakusita kuzungumzia utunzaji wa vifaa vya muziki kwa kila kikundi kilichopo mahali hapo kuboresha uhifadhi wa vyombo ili kuondoa tatizo la kupotea na kupoteza ubora kabla ya wakati.
     Bw Ezekiel Mwaja ambaye ni mmoja wa mafundi mitambo wa huduma alisema"Hilo ni jambo zuri kwani umakini utaongezeka zaidi na kila mmoja atakuwana uwezo wa kuendesha mitambo ya muziki na kuitengeneza ikiharibika kuliko kutafuta fundi kutoka nje ya huduma"alisisitiza akiungwa mkono na wenzake wengi.Hata hivyo baadhi ya walimu wa vikundi walifurahia jambo hilo na wanalisubiri kwa hamu na watatoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha  zoezi hilo.
      Wito wa kumsifu Mungu umekuwa ukitolewa mara kwa mara na Wainjilisti wa Huduma ya Uinjilisti  na Maombi Nyumba kwa Nyumba kutokana na kuwepo kwa upungufu wa waimbaji kwenye kwaya na bendi zinazohudumu mahali hapo hivyo kiwango cha uimbaji na kumsifu mungu kupungua.