Friday, January 18, 2013

WAKRISTO WAASWA KUTOKUTEGEMEA MISAADA KUTOKA MAKANISANI.

WATAKIWAKUJIAJIRI WENYEWE ILI KUJIKWAMUA NA UMASKINI
Mwinjilisti Reuben Mhuza (Kushoto) kutoka  Huduma ya Uinjilisti na Maombi  Nyumba  kwa Nyumba  akisisitiza jambo wakati wa semina ya kiroho na ujasiriamali iliyofanyika Muheza Mkoani Tanga (kulia) ni Kenoni Mnubi akimsikiliza kwa makini. Picha Na Onesmo Abraham 

Na Onesmo Abraham
     Wakristo nchini wamaetakiwa kujituma kwa kujikita katika shughuli za ujasriamali ili kuondokana na mfumo wa kutegemea kuomba misaada kutoka makanisani na kwenye taasisi mbalimbali kwani kufanya hivyo kutwawadumaza wao pamoja na kanisa.Hayo yamezungumzwa na Mwinjilisti Reuben Mhuza kwenye semina ya neno la mungu pamoja na ujasriamali iliyoandaliwa na Huduma Ya Maombi Na Uinjilisti Nyumba Kwa Nyumba Tanzania iliyofanyika mkoani Tanga katika wilaya ya Muheza.
      Akizungumza wakati wa semina hiyo amesema kumekuwa na mzigo mkubwa kwa kanisa na hata serikali  kwa kutumia fedha nyingi kuwasaidia watu ambao wanauhitaji lakini wanauwezo wa kufanya kazi huku wengine wakiomba mikopo makanisani kwa ajili ya biashara lakini huzielekeza kwenye shughuli nyigine ambazo haziwezi kuwaingizia kipato na kushindwa kurejesha mikopo waliyokopa hivyo kulifisi kanisa na wenyewe kubaki maskini,alisema,"Watu wengi wamekuwa wanachukua mikopo bila kuweka malengo na mwisho kujikuta hawajafaidika na chochote zaidi ya kujiongeza madeni hivyo hakikisheni mnapo kopa mna malengo ilikuzalisha zaidi kuliko kupoteza" alisisitiza
      Kwa upande mwingine elimu ya ujasiriamali iliyotolewa na kwenye semina hiyo iliashiria kuwafungua ufahamu wakazi wa Muheza na kuazimia kuanza kutumia mbinu mbalimbali za kijasiriamali ikiwemo ya kujiajiri wenyewe na kujiunga na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali wilayani hapo.Na baadhi ya washiriki kwenye semina hiyo walielezea jinsi walivyoguswa na elimu waliyoipata Bi Nagendagenda ni mmoja ya washiriki alikuwa na haya ya kusema"Mimi sikuwa na elewa kuhusu mikopo na nilikuwa najua mpaka mtu ajiajiri mpaka awe na prsa nyingi kumbe hata ukiwa na mtaji mdogo ila ukausimamia vizuri unaweza kupiga hatua kubwa na kumiliki biashara kubwa na ahidi kuwa mwalimu kwa wenzangu ili umasikini tuutupe mkono" alibainisha.
     Huduma ya Uinjilisti na Maombi Nyumba Kwa Nyumba iliandaa semina hiyo iliyoenda sambamba na neno la mungu ambalo lilifindishwa na Mwinjilisti Paul Nnwani pamoja na Mwinjilisti Reuben Mhuza ikiwa na lengo la kutoa elimu ya kiroho na stadi za maisha kwa jamii pamoja na wafuasi wa huduma hiyo ilifanyika wilayani Muheza ilidumu kwa muda wa siku tatu ilihudhuriwa na mamia ya wakazi waliokaribu na eneo hilo pamoja na sehemu mbalimbali za jiji la Tanga imeonekana mkombozi na dira kwa wakazi wa Muheza kutokana na kufunguliwa kielimu kuhusu suala la ujasiriamali na stadi za maisha.

No comments:

Post a Comment