Tuesday, March 26, 2013

HATUA MUHIMU ZA KUKUA KIROHO


CHUKUA HATUA

MWINJILISTI  PAUL
Joshua 3:1-5 Joshua anawaambia wana wa Israeli kuchukuwa hatua ili kuweza kukabili safari  iliyokuwa mbele yao kwa kuwa  wanatakiwa wajitakase  ili waweze kuanza safari.ili uweze kufanikiwa ni lazima uchukue hatua ya kutenda au kukabili jambo husika ambalo unatalaji kulifanya,hivyo tunatakiwa tuchukue hatua katika neno ili tuweze kushinda vita vinavyo tukabili ,na Mungu anatusubili sisi aone kama tunatii neno lake kwa kuchukua hatua ili aweze kushusha Baraka zake juu yetu.
Kutoka 2:11-15 Jitahidi kuangalia hali uliyokuwa nayo  kisha angalia yale unayoyafanya  kama kweli yanaendana na neno la Mungu linavyotuonya na kutufundisha,na kama sivyo  basi chukua hatua ya kujirekebisha ili Mungu akutendee,wakristo wengi wanajifariji  kwa kuomba maombi marefu, kuhudhulia  kwenye ibada kila siku,lakini wanasahau kuwa Mungu anapendezwa na wanaotii neno lake na kukubali kutubu,kwa kughaili na kuacha maovu na kutenda mema.Kutoka 3:6 acha kujifariji kwa kuigawa dhambi ukidhani kuna kubwa na ndogo,elewa  kwa Mungu zote ni dhambi kwa kuwa zinampeleka mtu jehamu.Kutoka 5:1 licha kuwa  utachukuwa hatua  sio  kwamba mambo yatakuwa mazuri  hapana, inawezekana yakawa magumu sana ,kama ilivyokuwa kwa Musa na Haruni wakati Mungu anasema nao juu ya kwenda kwa Farao kuomba kibali cha wana wa Israeli  kwenda kumwabudu Mungu wao.kutoka 5:1-12 tunapochukuwa hatua bwana anajidhibitisha kwetu,zipo hatua zinazotufaa sisi tuzichukue ili kuweza kupona.
·                            Chukua  hatua ya kuliamini neno la Mungu.Kutoka 14:13-16,wakristo walio  wengi wanashidwa kwa kuwa wanakuwa mafundi wa kusikiliza na kuandika mafundisho yote yanayofundishwa,lakini  ndani yao kumejaa mwalakini na kutoamini kuwa maneno  yanayosemwa au ahadi zilizotolewa na Mungu kuwa ni kweli ,tunakuwa wagumu wa kuamini  tunasubili mpaka tuone ndipo tuamini ,yapo mengine hatutapokea endapo hatutaruhusu  kuamini ndani yetu.
·                       Chukua hatua ya kutenda.yapo mafundisho ya Mungu ambayo yanatufundisha  kuamini neno la Mungu ili tuweze kupokea Baraka ,lakini waliowengi ndani yetu tumekuwa na mashaka juu ya kile ambacho tunakiomba na matokeo yake watu hawapokei kwa kuwa ndani yao yamejaa mashaka  mengi.Musa anaambiwa na Mungu juu ya kuwaongoza wana Israeli afanye tendo la imani la kupiga fimbo juu ya bahari na Musa alipochukua hatua bahari iligawanyika na wakapita salama,je? endapo angekuwa na mashaka wangevuka? Matendo 12:1…,Hesabu 13:1-3
·                      Chukua hatua ya kuhakikisha  kile unachoambiwa.katika nyakati hizi  tulizo nazo ni ngumu na mbaya sana kama hatutachukuwa hatua  za kumkariba Mungu ili atusaidie,kwa sasa  wapo watu wanaojiita kuwa ni manabii na  mitume na mafundisho wafundishayo  siyo mazuri kwetu ,hivyo inatakiwa  kuhakikisha kile unachojifunza kama kweli ni chema mbele za Mungu na utaweza kuhakikisha kwa kusoma neno na kumruhusu roho mtakatifu atufunulie na kutufundisha.
·                   Chukua hatua ya kumng’ang’ania Mungu Kutoka 33:1-6 licha ya kuwa Musa  alimg’ang’ania Mungu si kwa kutaka mahusiano mema na Mungu bali alitaka pia ushilika na yeye,hivyo na wewe usikubali  kuondolewa au kujiondoa  mbele za Mungu  pasipo kupokea kile ambacho  umeahidiwa wewe ukipate,ng’ang’ania kwa Mungu ili ashilikiane nawe katika hali zote na majira yote na yeye  endapo utayatoa maisha yako kwake, atakupa yale yanayokufaa.
Joshua23:6 inawezekana kabisa imani zetu ni kubwa sana  lakini kama katika matendo hatufanyi inavotupasa basi imani zetu ni mfu,kwa kuwa neno la Mungu linasema imani pasipomatendo imekufa,Yakobo 2:14,17 unaposikia  neno la Mungu  epuka mizaha na kulichukulia mazoea  na uchukue hatua ya kulitendea kazi ,kwa kuwa kuna mambo huwezi kupata au hayawezi kuondoka yenyewe usipochukua hatua wewe mwenyewe,na ukichukua hatua Mungu ni mwema kwetu atatutendea na atatupa Baraka.Ameen.

No comments:

Post a Comment