Saturday, November 17, 2012

MABADILIKO YA ANZA HUMANN 2012\2013

Mzee Cyprian Sallu Kiongozi wa Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba Tanzania
HUDUMA YAPANIA KWENDA NA WAKATI ILI KUKIDHI HAJA ZA WAUMINI.

  Huduma ya maombi na uinjililisti nyumba kwa nyumba imedhamiria kwa dhati kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa uendeshwaji na muonekano kwa ujumla kuanzia mwaka 2013 ilikwenda sawa na technolojia ya kisasa,ambayo itafanya huduma hii kutambulika kitaifa na kimataifa jambo ambalo litasaidia kukua na kuokoa roho za watu kwa kuweza kuwafikia mahali popote.
   Akitangaza mabadiliko hayo ambayo yameonekana kusubiriwa kwa hamu na wafuasi wa huduma hii kiongozi wa huduma Mzee Cyprian Kizumba Sallu wakati wa ibada alisema"Kutokana na hali ilivyo tumeamua kufanya mabadiliko kwa kuweka idara mbalimbali kama idara ya habari,fedha,uinjilisti na idara ya ustawi wa jamii itakayo hakikisha kila mkristo anishi kwa usawa na kufuata maadili"alisisitiza
     Aidha mabadiliko mengine yaliyofanyika na pamoja kutokuwepo kwa ibada ya jioni siku ya jumatatu na ibada siku ya jumapili itakuwa ikianza mapema saa nane mchana ikiambatana na semina,huku maombezi yakiendelea kama kawaida.Sababu nyingine ni kuwapa watumishi wa mungu muda mzuri wa kufunga na kuomba pamoja na kuandaa masomo ya kufundisha wakati wa ibada.
      Hata hivyo moja ya mkakati ambao unatarajiwa kutumia gharama kubwa ni ujenzi wa jengo jipya la kuabudia [Safina] utakao gharimu mabilioni ya shilingi hivyo kiongozi huyo wa huduma akitoa wito kwa kila anayeguswa na jambo hili kuchangia chochote kwani uongozi pekee hauwezi kukamilisha ujenzi huo bila msaada kutoka kwao.
      Vilevile baadhi ya waumini wa huduma hii wameelezea jinsi walivyofurahishwa na mabadiliko hayo miongoni mwao ni  Bw Joseph Charles alisema"Kwa mabadiliko haya lazima neno la mungu lifike hata sehemu za mbali popote duniani maana kwasababu huduma imefungua tovuti ambayo itamuwezesha mtu yeyote  hata anaekuwa nje ya nchi kupata mahubiri kwanjia ya mtandao kwahiyo ni neema kubwa"alisema. 
        Ni miaka 39 imepita tangu kuanzishwa kwa Huduma ya Uinjilisti na Maombi Nyumba kwa Nyumba na mtumishi wa Mungu Hayati Edmund John ikiwa na lengo la kueneza injili kwa kila mtu bila kubagua dini,dhehebu wala jinsia.Hivyo mabadiliko hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kusherehekea miaka 40 ya huduma hii chini ya kiongozi wake wa sasa Mzee Cyprian Kizumba Sallu.

1 comment:

  1. Ni jambo zuri,Mungu azidi kuibariki huduma hii

    ReplyDelete