Saturday, November 17, 2012

WAFUASI WAOMBA RATIBA YA iBADA ISIBADILIKE.

Mzee Cyprian Kizumba Sallu,Kiongozi wa Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba   Tanzania
WATAKA IBADA ZIENDELEE KAMA KAWAIDA.

      Wakati kiongozi wa Huduma ya Maombi Na Uinjilisti Nyumba Kwa Nyumba Mzee Cyprian Sallu akitangaza kuwepo kwa mabadiliko na utaratibu mzima wa ibada za kila siku katika huduma hii kwa mwaka wa 2013 mambo yamekuwa tofauti baada ya wafuasi wa huduma hii kutoa maoni yao ambayo yalitofautiana na mtazamo wa uongozi wa huduma juu ya mabadiliko ya ratiba na ibada zinazofanyika kila siku kwenye makao makuu ya huduma hii Buguruni Malapa jijini Dar es laam.
     Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti bila kutaja majina baadhi yao walisema kuwa sababu kubwa inayowapelekea kutaka ratiba ibaki vilevile kama zamani kwasababu Kila mtu anasiku yake ya kuja kuabudu na kuna wengine hawana nafasi siku zingine kwahiyo wanaitumia siku ya Jumatatu ambayo ilikuwa iondolewe kwenye ratiba kusali na kupeleka haja zao kwa mungu hivyo wanaomba siku hii isiondolewe kwenye ratiba.Vilevile sababu zingine walizotoa walisema kumuabudu mungu hakuna likizo wala kupumzika hivyo wako tayari kuendelea na utaratibu uliokuwa mwanzo.
       Hata hivyo kiongozi wa huduma umekubaliana na matakwa ya wafuasi wake na kutangaza utaratibu ule wa mwanzo kuendelea alisema"Kutokana na maoni ya wenye huduma ambao ni ninyi wenyewe tumeona siku ya jumatatu ibaki pale pale hivyo ibada zitaendelea kama kawaida "alisistiza.Aidha kiongozi huyo amewataka wahubiri wajipange vilivyo na wajitahidi kuendana na ratiba kama kawaida na kuandaa masomo ya kutosha kila siku ilikuhakikisha watu wanapata kile wanacho hitaji na mungu awatie nguvu .
         Mabadiliko yaliyokuwa yamependekezwa ni pamoja na ibda siku ya jumapili kuanza saa nane mchana na kuisha saa kumi na moja na nusu jioni pamoja na kuundwa kwa idara mbalimbali kwaajili ya kuboresha mwenendo wa huduma utakao endana sawa na sayansi na teknolojia iliyopo sasa.Aidha malengo mengine yaliyopo kwenye ratiba ya kuanzia waka 2013 ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la kisasa la kuabudia litajkalo gharimu mabilioni ya shilingi hivyo wafuasi wa huduma wameombwa kujitolea kukamilisha  ujenzi huo kwa hali na mali.
 

No comments:

Post a Comment