Sunday, November 18, 2012

MKUTANO WA THE BIG HARVEST 2012 MKOANI TANGA KATIKA PICHA

Mpiga Drums wa kwaya ya Maranatha kutoka tawi la Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba Dar es laam akijiandaa kupiga kwenye mkutano wa The Big Harvest 2012 uliofanyika mkoani Tanga Muheza

Waimbaji wa kwaya ya Huduma ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba kwa kanda ya Tanga Mheza wakiimba katika mkutano wa The Bug Harvest 2012 uliofanyika mkoani humo

Kiongozi  wa Huduma ya Uinjilisti na Maombi Nyumba kwa Nyumba mkoani Tanga akifanya maombi kwenye mkutano wa The Big Harvest 2012 uliofanyika wilayani Muheza.


Waimbaji wa kwaya ya Maranatha wakicheza na kuimba kwenye mkutano wa The Big Harvest uliofanyika Muheza Mkoani Tanga         

Saturday, November 17, 2012

MABADILIKO YA ANZA HUMANN 2012\2013

Mzee Cyprian Sallu Kiongozi wa Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba Tanzania
HUDUMA YAPANIA KWENDA NA WAKATI ILI KUKIDHI HAJA ZA WAUMINI.

  Huduma ya maombi na uinjililisti nyumba kwa nyumba imedhamiria kwa dhati kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa uendeshwaji na muonekano kwa ujumla kuanzia mwaka 2013 ilikwenda sawa na technolojia ya kisasa,ambayo itafanya huduma hii kutambulika kitaifa na kimataifa jambo ambalo litasaidia kukua na kuokoa roho za watu kwa kuweza kuwafikia mahali popote.
   Akitangaza mabadiliko hayo ambayo yameonekana kusubiriwa kwa hamu na wafuasi wa huduma hii kiongozi wa huduma Mzee Cyprian Kizumba Sallu wakati wa ibada alisema"Kutokana na hali ilivyo tumeamua kufanya mabadiliko kwa kuweka idara mbalimbali kama idara ya habari,fedha,uinjilisti na idara ya ustawi wa jamii itakayo hakikisha kila mkristo anishi kwa usawa na kufuata maadili"alisisitiza
     Aidha mabadiliko mengine yaliyofanyika na pamoja kutokuwepo kwa ibada ya jioni siku ya jumatatu na ibada siku ya jumapili itakuwa ikianza mapema saa nane mchana ikiambatana na semina,huku maombezi yakiendelea kama kawaida.Sababu nyingine ni kuwapa watumishi wa mungu muda mzuri wa kufunga na kuomba pamoja na kuandaa masomo ya kufundisha wakati wa ibada.
      Hata hivyo moja ya mkakati ambao unatarajiwa kutumia gharama kubwa ni ujenzi wa jengo jipya la kuabudia [Safina] utakao gharimu mabilioni ya shilingi hivyo kiongozi huyo wa huduma akitoa wito kwa kila anayeguswa na jambo hili kuchangia chochote kwani uongozi pekee hauwezi kukamilisha ujenzi huo bila msaada kutoka kwao.
      Vilevile baadhi ya waumini wa huduma hii wameelezea jinsi walivyofurahishwa na mabadiliko hayo miongoni mwao ni  Bw Joseph Charles alisema"Kwa mabadiliko haya lazima neno la mungu lifike hata sehemu za mbali popote duniani maana kwasababu huduma imefungua tovuti ambayo itamuwezesha mtu yeyote  hata anaekuwa nje ya nchi kupata mahubiri kwanjia ya mtandao kwahiyo ni neema kubwa"alisema. 
        Ni miaka 39 imepita tangu kuanzishwa kwa Huduma ya Uinjilisti na Maombi Nyumba kwa Nyumba na mtumishi wa Mungu Hayati Edmund John ikiwa na lengo la kueneza injili kwa kila mtu bila kubagua dini,dhehebu wala jinsia.Hivyo mabadiliko hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kusherehekea miaka 40 ya huduma hii chini ya kiongozi wake wa sasa Mzee Cyprian Kizumba Sallu.

WAFUASI WAOMBA RATIBA YA iBADA ISIBADILIKE.

Mzee Cyprian Kizumba Sallu,Kiongozi wa Huduma Ya Uinjilisti Na Maombi Nyumba Kwa Nyumba   Tanzania
WATAKA IBADA ZIENDELEE KAMA KAWAIDA.

      Wakati kiongozi wa Huduma ya Maombi Na Uinjilisti Nyumba Kwa Nyumba Mzee Cyprian Sallu akitangaza kuwepo kwa mabadiliko na utaratibu mzima wa ibada za kila siku katika huduma hii kwa mwaka wa 2013 mambo yamekuwa tofauti baada ya wafuasi wa huduma hii kutoa maoni yao ambayo yalitofautiana na mtazamo wa uongozi wa huduma juu ya mabadiliko ya ratiba na ibada zinazofanyika kila siku kwenye makao makuu ya huduma hii Buguruni Malapa jijini Dar es laam.
     Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti bila kutaja majina baadhi yao walisema kuwa sababu kubwa inayowapelekea kutaka ratiba ibaki vilevile kama zamani kwasababu Kila mtu anasiku yake ya kuja kuabudu na kuna wengine hawana nafasi siku zingine kwahiyo wanaitumia siku ya Jumatatu ambayo ilikuwa iondolewe kwenye ratiba kusali na kupeleka haja zao kwa mungu hivyo wanaomba siku hii isiondolewe kwenye ratiba.Vilevile sababu zingine walizotoa walisema kumuabudu mungu hakuna likizo wala kupumzika hivyo wako tayari kuendelea na utaratibu uliokuwa mwanzo.
       Hata hivyo kiongozi wa huduma umekubaliana na matakwa ya wafuasi wake na kutangaza utaratibu ule wa mwanzo kuendelea alisema"Kutokana na maoni ya wenye huduma ambao ni ninyi wenyewe tumeona siku ya jumatatu ibaki pale pale hivyo ibada zitaendelea kama kawaida "alisistiza.Aidha kiongozi huyo amewataka wahubiri wajipange vilivyo na wajitahidi kuendana na ratiba kama kawaida na kuandaa masomo ya kutosha kila siku ilikuhakikisha watu wanapata kile wanacho hitaji na mungu awatie nguvu .
         Mabadiliko yaliyokuwa yamependekezwa ni pamoja na ibda siku ya jumapili kuanza saa nane mchana na kuisha saa kumi na moja na nusu jioni pamoja na kuundwa kwa idara mbalimbali kwaajili ya kuboresha mwenendo wa huduma utakao endana sawa na sayansi na teknolojia iliyopo sasa.Aidha malengo mengine yaliyopo kwenye ratiba ya kuanzia waka 2013 ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la kisasa la kuabudia litajkalo gharimu mabilioni ya shilingi hivyo wafuasi wa huduma wameombwa kujitolea kukamilisha  ujenzi huo kwa hali na mali.
 

Friday, March 16, 2012

HOUSE TO HOUSE EVANGELICAL & PRAYER MINISTRY

HUMANN: HUDUMA YA UINJILISTI NA MAOMBI NYUMBA KWA NYUMBA
means House to House Evangelical and Prayer Ministry.

This Ministry was founded way back in 1973 by the Late man and servant of GOD Evangelist Edmund John.
HUMANN Ministry is not a CHURCH but an evangelical and prayer ministry with special emphasis in sharing GOD'S unconditional LOVE to all people as exhibited in St. Mathew 11:28
"You will know the truth, and the the truth will set you FREE as is in St. John 8:32
To fulfill this mission HUMANN is reaching people through House to House Prayers, seminars, counselling, gospel preaching and prayers to all in need. We are located at Ilala, Buguruini Malapa, Dar es salaam. Behind Buguruni Hostels , adjacent to St. Mark Theological College/ St. John University College.
You are most welcome.
OUR SERVICES
EVENING
DAYS: Monday, Tuesday, Thursday, Friday and Sunday  TIME; 5:00 pm to 6;30pm

MORNING
DAYS: Monday, Tuesday, Wednesday, Thursday, Friday, Saturday  : TIME: 6;30am to 7:00 am

SUNDAY MORNING we allow our congregation to go back to their CHURCHS' denominations.


SEMINARS
DAY: Saturday only TIME 10:00am to 12:00pm

OUR EVANGELISTS. AND OUR PRAYER SESSION








 OUR CONGREGATION AND CHOIR