Sunday, February 24, 2013
Friday, February 8, 2013
UPATANISHO
Yohana 14:23,24
Makao ni sehemu au mahali palipotengenezwa ili kitu au kiumbe kiishi.,Neno la Mungu linasema kuwa sisi
ni makao yake Yesu kristo.Yohana15:5
nyakati hizi ambazo kibiblia zinaonekana kuwa ni za mwisho wanadamu wameamua kumfukuza Yesu ndani yao na kuruhusu
Yule roho asi ambaye ni shetani. Yohana15;7 anasisitizia umuhimu wa sisi
kuwa makao na anaahidi kutufanyia yale
yote tunayomwomba tukiamini kwa jina lake atatupa.Moja ya sababu zinazoleta shida ndani ya mioyo ya wanadamu
ni kutokuwa na Mungu ndani yetu, na hili linawapata wakristo wanaojichanganya,ambao
kanisani kuingia kwao ni desturi dini wanaziheshimu wakiingia kanisani wanasifu, sadaka na michango mbalimbali wantoa lakini
bado hawaamini uweza wa kriso ndani yao,na kristo mwenyewe ndani yao hayumo.
Kupitia neno la
Kristo anasema neno lake likikaa ndani yetu na yeye atakaa ndani yetu,na
kupitia neno la Mungu unamruhusu Yesu mwenyewe aje kukaa na wewe.jitahidi kila
neno linapokuja kwako uliruhusu likae ili kristo akae na wewe.Yohana 6:63’’Roho ndiyo itiayo uzima mwili
haufai kitu’’ Ufalme wa Mungu umeenea kila mahali na wakristo wameukataa na kuutupilia mbali
,ndiyo maana utashuhudia maajabu mengi ya kushangaza wanayafanya wakristo na
siyo wapagani.Yohana 6:64.Kuamini ni
kusadiki na kusadiki ni kuwa ni mmja wa waliosikia,wakristo wengi licha ya
kushuhudia na kuona mambo makuu wanayotendewa na Mungu bado
kuamini kwao kuko mbali kwamaana
hiyo wamempa nafasi shetani ya kukaa
kwao.Na kama hulisikii neno la Mungu
juwa wazi kuwa sauti utakazozisikia ni zashetani kwa kuwa zipo njia zilizompa uhalali wa yeye kukaa kwako na Mtu anaye tumkishwa na shetani anaweza kuwa
mchawi hata bila yeye kujua.
,Kutoka 22:18 ,19.
Maana mchawi kila akikaa anakuwa na hamu ya kuwaua wenzake na huyu siku zote anamuhusu shetani na ameshampa kibali cha kukaa ndani
yake.Wakristo wengi licha na kumshuhudia Kristo katika maisha yao bado
wanaendelea kutambikia na kutoa kafara
mbalimbali kwa shetani na maagano haya yanawapatanisha na shetani ndiyo yanayomfanya ibilisi apate nafasi ya kukaa ndani yetu na
kutumiliki .Kumb18:22.
Wapo manabii na watumishi ambao shetani ndani yao ameweka pepo saba za utambuzi na
wamekuwa wakiwapotosha walio wengi wakidhani kuwa ni Mungu aliyejiinua,na ili
kuziepuka roho hizi ni kuwa mtu wa
kusali na kuomba ili Mungu mwenyewe ajidhihirishe kwako.Kumb 5:7,jambo linalotupoteza wakristo wengi ni juu ya kusikiliza mafundisho na mafunuo ya Miungu
au ya watu ambao wanakaa na
shetani na roho hizo za uasi zinakaa ndani yao.Katika maandiko Mungu anazungumza
juu ya kujua mti wa mema na mbaya ambao
ni uhalali wa kufanya uchaguzi ,ikifika
mahali ndani yako ukaanza kusikia hali
ya kuwachukia watumishi bila sababu yoyote
jua ndani yako shetani ameshapata
nafasi,na kazi kubwa ni kuondoa kuamini kile Kristo alichofanya ndani yetu,na
ukiona hivyo basi omba ibada ya upatanisho na Mungu ili Kristo aweze kutukuzwa
ndani yako.
Wakolosai 1:21
Neno linasema kuwa ni Yesu
awezaye kutupatanisha na Mungu baba kwa njia ya neno lake,Wapo
wakristo wengi wanafanya dhambi kwa siri
wakiwaficha wachungaji wao,wakristo wenzao na kusahau kuwa hao ni wanadamu na
hawana mbingu ya kuwapeleka,na neno linatuweka wazi kuwa Mungu huichunguza mioyo na viuno vyake na
kwake hakuna siri kwa kuwa anajua kesho
na keshokutwa ya mwanadamu.Dhambi hizi
anazofanya mwanadamu ndizo zinasababisha
asipokee baraka,(Yeremia 48:7-8
)kwa maana hiyo ukiruhusu dhambi wewe mwenyewe kwa makusudi jua wazi kuwa
huwezi kumwona Mungu wala kupokea Baraka kutoka kwake.
Kwa maana hiyo muombe Roho mtakatifu akukumbushe dhambi ulizozifanya aidha wakati unajua au hujui,ili kwamba uweze
kufanya matengenezo ya maisha yako ili
uweze kujenga mahusiano mema na Mungu baba ambaye neno linasema kuwa ni mwema
wa yote lakini pia ni mwingi wa rehema,na huwanyeshea mvua walimao na
wasiolima,kwa maana hiyo hana ubaguzi wa mtu, ukitubu yeye ni mwema anasamehe
na kusahau kabisa.Basi msihi roho mtakatifu aliyeko ndani yako aendelee kufanya
mabadiliko ndani yako na Yesu mwenyewe aweze kukaa kwako milele.
Mungu akubariki sana.
:SIRI ILIYOKO KATIKA MWILI,NAFSI NA ROHO
Na Mwinjilisti Reuben |
Tumwombe Mungu atujalie kuyajua mapenzi yake ,tabia yake namna mpangilio na mapenzi yake.Watu wengi wanajuhudi katika Mungu lakini hawana maarifa ya kumjua Mungu, kwamba tukienda kwake twende kwa namna gani ,kwamba yeye anatujua , lakini anatuona vipi hapo ndipo kuna ugumu.tunafika wakati tunamwona Mungu hawezi na hatusaidii ,kawaida huwezi kumfahamu Mungu ikiwa wewe mwenyeewe hujifahamu.
Huwezi
kumfahamu Mungu ikiwa wewe mwenyewe hujifahamu ulivyo mbele za Mungu,kwa kuwa
Mungu anasema tusafishe kabisa nafsi zetu ,mwili na roho pia kwa maana hiyo
tuna sehemu kuu tatu ambazo mwanadamu
anatambulikwa kwazo nazo ni mwil,nafsi na roho. katika mwili tunajitazama kwenye kioo kuweza kugundua kasoro tulizo
nazo,lakini katia nafsi tuna misisimko hisia pamoja na utashi,lakini katika roho tunalo neno la Mungu ambalo ndicho
kioo kinachotufanya tujitazame jinsi
tulivyo na tuweze kujifahamu kuwa ni wazinzi, waongo ,wafitini ,wambea.1Wathesalonike5:23”,Mungu wa amani mwenyewe
awatakase kabisa nanyi nafsizenu miili yenu
mhifadhiwe muwe kamili bila lawama wakati wa kuja kwake bwana wetu Yesu
kristo”.
Hivyo basi walio
wengi wanajua kuwa wameumbwa katika sehemu hizi tatu lakini hawajui kazi za Mwili,Nafsi na Roho na
kama hujui kazi hizo hilo ni tatizo kwa
kuwa mwili utauchafua roho na nafsi
vitashidwa kupokea Baraka na neema za
Mungu.Na endapo ukizijua kazi hizi wakati neno la Mungu likija kwako utagundua
kuwa neno hili limekuja kwaajili ya mwili nafsi au roho.1Wakoritho2:10-12.Upya unaosemwa katika biblia ni neno maana
anasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona,inamaanisha tumeponyeshwa roho na nafsi
na sio mwili,na kama Mungu ameshatupa inatakiwa sisi tupokee.
Yapo Mambo Manne ambayo Unapaswa Uyafahamu.
Mwili unapingana na roho.wagalatia
5:17 katika maisha kuna vitu ambavyo mwili unavitaka na roho haitaki, roho
inataka ila mwili hautaki,lakini ili uweze
kupata Baraka na neema za Mungu ongozwa
na neno na uifuate roho yako.Yohana6:63 .ukikubali
neno la Mungu likuongoze jua kuwa uzima
wa Mungu unao, lakini ukiongozwa na mwili lazima utashidwa kwa kuwa mwili
unatabia zake unania zake na na unamahitaji yake pia.tabia za mwili 1wakoritho3:1-3
-Ukiwa na tabia za
mwili huwezi kupata vitu vya rohoni,ni
lazima ujichuje kuingiakatika tabia
za roho ili uweze kupokea Baraka Wagalatia5:24
,Mwili una nia yake mawazo yake,na
maana ya nia ni mwelekeo wa kufikia hatma fulani kwa hiyo basi mwili
kuna sehemu unataka kufika na roho pia kuna sehemu inataka kufika.Warumi8:6-8 ,nia ya mwili ni katika
dhambi na nia ya roho ni kuiona
mbingu.Naomba uelewe kuwa mwili unatabia zake, kama vile ulevi uongo husuda, uzinzi na nyinginezo,na tabia za rohoni pia ni upendo, unyenyekevu,ukarimu
pamoja na nyinginezo,na mtu anayeishi katika haya ana matumaini ya kufika
mbinguni.
Unapokumbana na matatizo mpaka ukahisi mifadhaiko ya kumkufuru Mungu
,jifunze kwa waliopitia magumu na
wakashinda kama vile Ayubu3:2-11.Watu
wengi tunapokumbana na wakati mgumu ndipo tunapomwacha Mungu na kuangamia.jifunze
kwa Daudi pia 1samweli30:1-4,6 Daudi
alijitia nguvu katika bwana akashinda,na
wewe pia inatakiwa ujitie nguvu katika bwana.Wapendwa tuangalie jinsi ya
kujitia nguvu katika bwana ili na sisi tuweze kushinda.
1.Tengeneza mahusiano yako na Mungu.
Unapokumbana na
matatizo ukawa mtu wa kulaumu ,jua
unamchukiza Kristo zaidi amini kuwa
Mungu anakupenda sana zaidi ya unavyofikilia na anakuwazia mema wala siyo
mabaya,hivyo jitahidi utengeneze mahusiano yako na Mungu.Warumi8:35,zab 107:19-20, waebrania4:12
2.Tafakari na kumbuka
ahadi za Mungu.
Mungu alikuahidi nini katika
neno lake,Kumb20:1 jua kuwa
Mungu anasema na roho wala haihusiani na
milango ya fahamu iliyo katika mwili ni
tofauti kabisa.Yohana1:1…,11-12, kumb 8:18
3.Tengeneza picha kuwa kile ulichoomba umeshapokea.
Liamini neno la
Mungu na uwe na imani ya yale uliyoomba
kuwa umeshayapokea.Warumi4:20, 10:17
jitahidi ukuze kiwango cha imani yako kiwe juu.
4.Jizoeshe kuisemesha
nafsi yako.
Jitahidi
kuisemesha nafsi yako aidha ni kuikanya
au kuionya,kile ambacho Mungu anakituma kwako
kupitia neno lake hakikisha unakikubalisha katika nafsi na roho
yako,elemea mwili wako ili roho yako iinuliwe.
5.Jenga tabia ya
kufunga.
Jifunze kuwa na faragha na Mungu
katika hali ya kujinyima katika mwili kwa kufunga,Kufunga kumegawanyika katika
sehemu mbili,kunakufunga kuunyima mwili chakula,na pia mfungo wa aina ya pili
ni kufunga nafsi yako, yaani kuinyima nafsi yako kuhitaji na kutamani vitu
ambavyo mbele za Mugu ni vibovu.Na ukifunga kwa kusimama na neno la Mungu yeye
ni mwema atatenda sawasawa na alivyoahidi.
IMANI YAKO IPO WAPI?
Na Mwinjilisti Reuben |
Imani ni kuwa na hakika ya mambo ambayo hayajawa bado.Inatakiwa uione kazi,biashara na mafanikio ya maisha pasipo uhalisia kwa kufanya hivyo utakuwa umetimiza imani ya kufanikiwa hivyo utaishi maisha ya kumpendeza kwa kutarajia yale uliyoyaamini kama atakutendea.Mungu amegawa imani kwa kila mtu pia anataka imani iendelee kukua ili uvune Baraka kwake.(Warumi 12:3),. (Waebrania
11;6) tunaelezwa kuwa Kitu ambacho kinampendeza Mungu ni Imani ,kwa maana hiyo pasipo imani
hatuwezi kumpendeza Mungu. Kazi za shetani ni
kuiba,kuchinja na kuharibu lakini Bwana Yesu alikuja tuwe na uzima kisha
tuwe nao tele,shetani anatuibia,anachinja imani na kuharibu kwa kuwa anajua akifanya hivyo hautakuwa na
nafasi ya kumwamini Mungu.Imani ni kuwa na hakika ya mambo ambayo hayajawa
bado,inatakiwa uione kazi,biashara na mafanikio ya maisha pasipo uhalisia ,kwa
kufanya hivyo utakuwa umetimiza imani ya kufanikiwa hivyo utaishi maisha ya
kumpendeza kwa kutarajia yale
uliyoyaamini kama atakutendea.Mungu amegawa imani kwa kila mtu pia anataka
imani iendelee kukua ili uvune Baraka kwake.(Warumi 12:3),.
Kuna aina nyingi za imani lakini hapa tutazungumzia aina
tano,ambazo mara nyingi tunakutana nazo katika maisha yetu ya kiroho na
kimwili
.
01.Imani Iliyosukumiwa
mbali.
Hii ni imani iliyo
tupwa ,na kuna watu wengi wanaomuona Mungu kupitia ishara na miujiza lakini bado
hawamwamini kwa maana hiyo wanaitupa imani.Paulo anasema hawa wamekabidhiwa kwa
shetani ,na shetani akiwa kwako
uliyekuwa unamjua Yesu halafu ukamkana hali yako inakuwa mbaya kuzidi uliyokuwa
nayo mwanzo kwa sababu hata weza
kukutendea muujiza kwa kutokumwamini kuwa yeye anaweza.
02.Imani Iliyokufa.
Hii ni imani ambayo mtu anaamini kuwa Yesu yupo lakini
hatendi mema ,imani pasipo matendo imekufa,neno linahubiliwa lakini kile
kilichohubiliwa huendi kukitenda lakini kwa kawaida imani iliyo hai il itimie lazima ulichoelekezwa na neno la Mungu
inatakiwa ukifanye.Neno la Mungu linatuagiza kuwa tusiogope kwa kuwa aliye
ndani yetu ni mkuu zaidi kuliko vyote,hivyo ondoka katika imani iliyokufa.
03.Imani ya Kweli.
Hii ni imani ambayo haina unafiki wowote wala uongo ndani yake,kwasababu imani
yenye unafiki ni yakuigiza wala siyo ya kweli na kuna watu ambao
wanayo.Wanahofu ya kibinadamu wala hawana hofu ya kimungu.Imani ya kweli
inasifa hizi;
-Inamtazama Yesu
-Inakiri
haimwonei aibu Yesu.
-Inatuliza moyo haina jaziba
04.Imani Haba.
Ni imani ndogo sana,hii inatilia shaka juu ya mahitaji ya
mwili lakini neno la Mungu linasema
atatupa vyote kwa kuwa hata tukijisumbua hatuwezi kuongeza hata urefu wa
kimo cha mkono wetu.ikitokea dhoruba inatoweka.(Mathayo 8:26) na wakati wa matatizo imani hii inadhihilika kwa
sabababu inamezwa na matatizo.(Mathayo
14:30) Petro alikuwa na imani lakini alipoingiza mashaka ndani yake ndipo
alipoanza kuzama,jitahidi shida na matatizo uliyonayo yasikuzidi uwezo maana
yanaweza kukuzamisha .
Pia imani hii
inasahaulisha mambo makuu aliyokutendea Mungu(.Mathayo16:9-10) usiwe na imani haba unapokumbana na
matatizo,tafakari ni yapi uliyovushwa kwa neema
ndipo ujitie nguvu usonge mbele.
05;Imani Kuu.
(Mathayo 8;8-10),
Ukitangaziwa uponyaji aminikuwa umepona,hii ndio maana ya Imani Kuu ya
kutegemea neno la Mungu na kulifanyia kazi ,zifuatazo ni sifa za Imani Kuu.
-Ukiing’ang’ania huwezi kumuacha Yesu( Mathayo 15 ;21-28).
Kuna watu wakiombewa wanakuwa wepesi wa kukata tama wakati
wa kusubiri majibu ya maombi yao hivyo ni heri kuvumilia kwasababu Mungu
antenda kwa wakati wake kwahiyo uwe na Imani kwa neno utakalosikia kutoka kwa
watumishi wa Mungu.
Ni wajibu na haki kwa kila mkristo anayemuamini Mungu kujihoji na kufahamu imani aliyonayo ni ipi na ipo kwenye kundi lipi,je ni Imani Haba,Imani iliyotupwa au Imani kuu, na kwakufanya hivyo kutatuweka katika nafasi nzuri kwenye mahusiano kati yetu wanadamu na mungu aliye mbinguni.
Tuesday, February 5, 2013
UBATILI MTUPU
Na Paul Nhwani.
Mhubiri 12:1-11
Mfalme Suleimani anashuhudia kuwa alikuwa na mali nyingi
pamoja na hekima ,lakini licha na hayo
bado akayaona yote kuwa na ubatili mtupu.licha ya hayo suleimani akaona
yote ni bule usipomcha Mungu.(Mhubiri
12:13),japo alilalamika sana lakini aligundua na kusema kuwa mwanadamu
lazima umche Mungu na umuhofu MUngu
pia.Suleimani baada ya kugundua kuwa ya
duinia yanapita akaona kuwa ni Ubatili ni vema kumjua Mungu.
Kwa hiyo
Mfalme Suleimani anatupa maana halisi ya Ubatili kuwa ni
kitu kisichokuwa na thamani ya kweli au ya kudumu,sasa jiulize hicho
unachosumbuka nacho kitakufikisha kwa
Mungu au ndio ubatili mtupu alioona Suleimani?Maisha yetu ni mjumuisho wa mambo
matatu yanayo tuzunguka ambayo ni ;MAWAZO,MANENO,MATENDO,NA
MWENENDO. Tunaweza tukashidwa kufikia hatma ya mafanikio ya kumwona Mungu
kutokana na mawazo maneno na matendo yetu kwa wennzetu endapo hatuwatendei
yaliyo mema.kutokana na wanadamu wengi kujipenda sisi wenyewe na kuthamini mambo
yetu,na kusahau kuwa Mungu ameagiza
tupendane zaidi, hata Yule ambaye kwako amekuwa ni kwazo kwako mara
nyingi unaagizwa kumpenda.
Mambo yafuatayo yanaweza kutufanya tusifikie hatima njema ya kumwona
Mungu na kujikuta tukibaki kujiita walokole bila kujua nini hatima yetu hapo
baadae katika maisha ya kiroho.
01; Mienendo yetu
mbele za watu na Mungu.
Mambo haya yanaweza
kuwa ubatili na kutufanya tushidwekufikia hatma njema ya kumwona Mungu.(Mathayo 6:1-2).Mahali pengine tunafanya vitu ili tusifiwe na
kuangaliwa na watu.Ukifanya hivyo jua
utapata malipo na thawabu za watu sio mbele za Mungu ,kwa hiyo tuangalie
mwenenendo na tabia zetu.
02.Wanadamu kuwa wasikilizaji wa neno na sio watendaji.
Watu waliowengi wanasikia na kuandika sana mafundisho ya
neno la Mungu lakini hawayatendei kazi.Neno la Mungu ni kioo cha rohoni ambalo
linatuonesha jinsi tulivyo,kwa maana nyingine linatuonesha maisha ya mahusiano yetu na Mungu.lakini
tumekuwa tukiyakimbia makusudi ya neno la Mungu juu yetu.Katika( Yakobo1:22-27). Tunaoneshwa kitu
kinachosababisha tushindwe ni kuwa wasikilizaji tu na sio watendaji hivyo ni
vizuri kila anaesikia neno la Mungu
kulifanyia kazi
03;Kuwa
watu wa kujihesabia haki na kuwahukumu
wengine.
Mambo ya
kuhukumu na kujihesabia haki, huo ni
ubatili mbele za Mungu .Mwinjilisti
Mathayo anasema (Mathayo 7:1-5),neno la Mungu linasema kuwa hatuna ruhusa ya kuhukumu,na ubaya wa ubatili
unakufanya ujione muda wote kuwa uko salama .Suleimani alikumbushwa na Mungu,lakini kama
asingekumbushwa na Mungu yamkini hata
sisi tusingepata nafasi hii ya kuoywa.
04.Kuishi maisha ya uchungu
na hasira.
Licha ya kuwa watu wengi
wanatendewa mambo makuu na Mungu ,bado ndani yao wanauchungu wa kutokuwasamehe wale waliowakosea.Hii inasababisha watu
wasizione Baraka za Mungu na kama tutadumu katika haya ya kutokusamehe hatuwezi
kufikia hatima njema ya kumwona Mungu
.Paulo anasema( Efeso 4:31-32).kusamehe
kunatakiwa ukate shauri la kumsamehe
mtesi wako,ili ufike hatma ya kumwona Mungu.
05.Kutokuwa na furaha katika Bwana.
Watu wengi furaha yao iko kwenye vitu,mali na katika matokeo
mazuri sana,ambayo wanatendewa na Mungu
na sio katika Kristo Yesu.Hivyo basi inatupasa
kujitahidi pasipo kujali kuwa ni mzima au ni mgojwa,umepata au
hujapata,umefanikiwa au hujafanikiwa,jitahidi mda wote furaha yako iwe kwa bwana.(Wafilipi 3:1).Tufurahi katIka
Bwana na sio katika vitu, hali au
matokeo mazuri.
06.Kutokuwa na
upendo.
Katika maandiko matakatifu tunaagizwa kuwapenda zaidi
wale ambao wako kinyume na sisi ,lakini tumeshidwa
kusimama sehemu hii zaidi tumewahukumu
wengine na kuwaona kuwa ni waovu.Fahamu kuwa hii inaweza ikasababisha usifikie hatma
njema,Kwa kuwa Mungu ambaye ndiye tunaemwamini
yeye mwenyewe ni upendo na
alitupenda sisi kwanza.(Mathayo 5:43-45)
utapata ukamilifu kwa kuwapenda
wasiokupenda ili upate thawabu
kwa Mungu wako,kwa kutokufanya hivyo
maisha yetu yatakuwa ni ubatili mtupu
.
07.Kujifanya kuwa tunampenda Mungu
kumbe ni uongo.
Waliowengi wanajifanya wanampenda Mungu sana lakini
wanayoyafanya ni mabaya,(Mathayo 15:7-9),angalia
na chunguza sana maisha yako .Mtu anaye mpenda Mungu haoni taabu kusoma neno lake, kutoa sadaka nzuri, na
kuonesha upendo kwa wenzake.hata kuweza kujitoa kwa wale wasiojiweza, wanaohitaji kama yatima wajane,pamoja na vikongwe
,tukifanya hivyo Mungu ataonekana kwetu na tutavuna Baraka.
Na hitimisho la haya yote
(Mhubiri 12:9) jichunguze
ndani ya nafsi ni lipi linaloweza kusababisha ubatili katika maisha yako na Mbele za Mungu
wako.Makusudi ya Mungu kwa wanadamu ni matatu (3) KUMJUA
MUNGU,KUMPENDA,NA KUMTUMIKIA
FAHAMU BAADHI YA TABIA ZA MWANADAMU
Na; Cyprian Sallu
Wapendwa katika maisha ya mwanadamu lazima kuwepo na mambo
mbalimbali ambayo yanaendana na maisha yake pamoja na mazingira ili kukamilisha
mfumo kamili wa maisha ya kiroho na kimwili.Hayo yote yaliyotajwa hapo yanaitwa TABIA.Tabia huleta picha kamilsi ya
mtu na mfumo wake wa maisha vilevile
hujulikana haraka sana kwa jamii inayozunguka eneo husika au mtu Fulani kwa
sababu wao ndio wanao kuona siku zote.Mara nyingi tumekwepa sana kutazama tabia
zetu na tukajishughulisha sana na mambo ya kanisa jambo ambalo husababisha
kutokea kwa dhambi.Lakini Tabia ya mtu si rahisi kubadilika mpaka Mungu mwenyewe ambadilishe na
amshuhudie kuhusu tabia yake.
Mtume Paulo alipewa neema na Mungu katika kujua tabia ya
wakristo huko Effeso na Korintho alibahatika kufahamu tabia na mwenendo wa wakristo katka kila kanisa kupitia njia ya roho,mafunuo .na shuhuda ndio
maana alisema, ‘’Sikuweza kusema nanyi kama watu wenye tabia ya rohoni bali kama watu wenye
tabia ya mwilini kama watoto wachanga
katika kristo’’.Alieleza hivyo kwa mtazamo wa tabia zetu sisi wanadamu na
maisha yetu kwasababu lazima kila mtu aishi chini ya mwongozo wa neno la mungu ili kwamba Tabia zetu ziwe za kiroho
na kuwa Baraka kwa wenzetu sio vikwazo.
Kutokana na hayo tabia ikajigawa katika makundi mawili TABIA NZURI NA TABIA MBAYA .Lakini pia katika hayo makundi mawili yanajumuisha aina zifuatazo za
Tabia katika maisha ya Mwanadamu ambazo zinahitaji utashi katika kufanya
uamuzi na kuishi kwa kuepuka vikwazo nza mitego ya shetani.
Aina za Tabia:
01.Tabia ya Kurithi:
Aina hii ya Tabia ni
vigumu kuifahamu na kuitambua endapo hutakuwa mfuatiliaji na usipo vunja laana
za ukoo maana hutokana na kurithi aidha kwa kupitia majina ya kurithi kutoka
kwa vizazi vyetu.Katika kurithi kunaweza kuwa na Tabia nzuri au Tabia mbaya ,
hivyo basi ni vizuri kila mzazi kuwa makini na kufuatilia kuhusu majina na vitu
ambavyo wanarithisha watoto wao.Mfano
wa tabia ambazo zinaweza kurithiwa,Uchawi,Uongo,Kiburi,Hasira na Nyingine
nyingi.
Umakini unahitajika katika kuepuka aina hii ya Tabia
kwasababu jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kurithishana hasa majina Mfano, Mtoto anaweza kuzaliwa akapewa jina
la babu yake lakini wazazi bila kufahamu
na kufuatilia historia ya mwenye jina wajikuta wamempa mtoto jina bila kuvunja
laana na kulitakasa jina lhilo upya ili mtoto asiweze kurithi hizo tabia za babu yake.Ni jambo gumu sana kwa mtu
asiyeamini na kufuatilia maandiko ya neno la mungu kwasababu laana imezungumzwa
katika biblia kuwa inaweza kumktesa mtu bila yeye mwenyewe kujua,unaweza kuona
mtu hafanikiwi au kila akifanya jambo haliendi vizuri anakimbilia kwa waganga
wa kienyeji akienda kusafisha nyota kumbe siri imejificha kwenye laana ya
kurithi jina la mtu wa zamani .Hivyo basi ni
vema kila mmoja kufuatilia asili ya jina lake na historia ya ukoo wake
ili kuepuka kuwepo kwa tabia za kurithi bila yakujua.
02.Tabia ya Kuiga
Tabia hii inakundi kubwa la watu wambao wameathiriwa
kwasababu ya mabadiliko ya mfumo wa maisha na utandawazi hasa vijana ambao hupenda sana kuiga Tabia ,mienendo na mifumo
ya maisha bila kufahamu hapo baadaye.Mara nyingi watu huiga kutoka kwa
marafiki,ndugu na jamaa kwa lengo la kuwaridhisha au kujiridhisha wenyewe
kwamba wanaenda na wakati lakini hawajui nini madhara ya kuiga.
1 Waebrania 13;17,
anatufundisha Tabia zitupasazo kuwa nazo kuwa tuwa tii wale wanaotuongoza tena
tuwaige na kufuata mienendo yao mizuri na ndio maana wakristo wengi wanabatizwa
majina ya watakatifu waliopita Mfano , Petro,Musa,Paulo,Mathayo na wengine
wengi.Vijana wengi wameingia katika kundi
hili la kuiga ilikuonekana wakotofauti na wengine lakini sababu kubwa ni
kutokulifahamu neno lamungu pamoja na historia ya ujana wa Yesu,hivi leo kijana
anaeokoka huonekana mshamba lakini
kijana aliyejiingiza kwenye kuiga mambo ya kigeni kama vikundi vya wacheza
disco,walevi na wahuni anaonekana wa maana kuliko Yule aliyeko kanisani.Ni
wakati wa kila kijana kujitambua na kijijengea tabia nzuri yenye misingi na
misimamo ya kiroho ili kujiwekea heshima kwenye jamii na maisha yake ya kiroho
yakiwa ushuhuda kwa kuutumia ujan wake vizuri bila kuiga mambo yasiyo na maana
mbele za Mungu .
Hata jamii nzima ya kitanzania imeanza kuiga utamaduni mbovu
kama ndoa za jinsia moja ambazo hazipo kwenye neno la Mungu na ni tabia ya
kishetani. Ni jukumu la watumishi wa Mungu
na wazazi kuwajengea watoto na kurekebisha tabia ya kuiga ,pia kuna baadhii ya
watumish nao wanaiga mambo jambo ambalo linahuzunisha na linapoteza heshima yao
katika utendaji wao kwasababu hakuna Nabii wala Mtume mwenye historia ya tabia
hii ya kuiga. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kujitengenezea na kufuata tabia za
kiutauwa na kuenenda akiwa ongozwa na
roho mtakatifu ili kuepuka kuiga mambo yasiyoendana na ukristo pamoja na
maagizo ya Mungu wetu vile vile ni heri kuiga mambo mazuri kuliko mabaya
03:Tabia Ya
Kuambukizwa:
Hii ni Tabia ya mwilini,katika amri zote mwanadamu anatakiwa
ajihadhari na mawasiliano ya mtu yeyoytekidamu ndio maana imeandikwa dhambi zote tunazofanya
ni makosa lakini dhambi ya uzinzi na uasherate ni dhambi ya damu
kuna kuambukizana tabia kuna kuambukiza hali mbaya .Enzi hizo wayahudi wakikuta
mtu anazini lazima apigwe mawe afe maana wamekwisha kuambukizana uzinzi natolea
mfano uzinzi na uasherati kwasababu ni dhambi ambazo zinaambukizwa kwa
kushawishiwa mtu hawezi kufanya akiwa
peke yake na zipo Tabia nyingi za kuambukizwa hivyo ni jukumu mkristo kutambua .
Ukahaba ni mmoja wapo ya tabia ya kuambukizwa |
Madhara ya tabia hii inaweza kukufanya ubaki pale pale
kimaendeleo unapoambukizwa dhambi au tabia yoyote ambayo sio nzuri ni vigumu
kutoweka katika mfumo wako wa maisha ,mara nyingi epuka kujichanganya kwenye
makundi ambayo hayana tabia kama yako kwasababu kinga ni bora kuliko tiba
hivyo jikinge juu ya watu wenye uwezekano wa kukuambukiza tabia mbaya . Hizo
ni baadhi ya Tabia za wanadamu tulio wengi ambao wakati mwingine tunaifanya
mioyo yetu kuwa migumu kwa kutokuiga mwenendo wa mungu aliyetuumba na kuacha
kuzifuata amri zake.Wakati mwingine tuna chelewa kupokea ahadi za mungu
kutokana na Tabia zetu kutokumpendeza yeye katika 2
Petro2 neno linasema kwamba bwana
hachelewi kutimiza ahadi zake na anaiona Tabia yetu sisi lakini anatuvumilia na
kutufundisha kupitia neno lake kuwa kama tabia zetu sio njema tufanye toba ya
kweli kwani tukifa katika tabia mbaya tutaingia katika hukumu.Ni lazima kila
mmoja achuchumilie kuishi maisha ya utauwa wa mungu na kujitahidi kuondoa Tabia
za mwilini ambazo zimepelekea kwa wakristo wengi kuyumba katika huduma
walizoitiwa na mungu.
Ili uwe na tabia nzuri au njema lazima upambane vizuri juu
ya roho na mwili maana roho hushindana na mwili maana wakati mwingine roho inaamsha
tama au vitu na tabia ambazo mwili hauzitaki lakini mara nyingi wakristo
tumeshindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi na kufuata tama za mwili na kuwa
maajenti wa shetani bila kujua kutokana
na kuingiwa na roho chafu kwasababu ya Tabia zetu tulizo nazo.Shetani amekuwa
macho akitazama Tabia zetu hivyo akiona tabia yako mbovu anaingia kwa
urahisi vile vile jinsi tabia yako ilivyo kutakufanya uingie jehanamu au
uzimani.
Dawa Ya Tabia Mbaya:
Tabia mbaya inabadilishwa na Neno la Mungu likiingia ndani ya moyo wa mwanadamu linasafisha
na kuondoa roho ngeni na Tabia zake jambo
ambalo hutokea baada ya wewe mwenyewe kuamua kumpa Yesu maisha yako na
kukubali kuwa neno la Mungu ni dawa na suluhisho la shida zako.
Yesu ni dawa ya tabia mbaya ukiamini na kufuata neno lake... |
Wito Kwa Wote;Wakati wote tukumbuke mwanadamu aliumbwa na Mungu
hivyo ni lazima afanye na kufuata mapenzi na amri za mungu ili asimuudhi tena
tusiweke ushabiki katika kumtafuta mungu na ufalme wake lakini kwa wakati huu
Wainjilisti,Wachungaji Na Wanaojiita Manabii wamekuwa na Tabia ya kujitwalia utukufu
kwamba wao ndio wanamtuma Mungu na wanaponya wagonjwa, kutoa pepo kwa nguvu zao
jambo ambalo halileti picha nzuri kwa watu mnao waongoza pia kuibua kiburi cha
imani kati ya dhehebu na dhehebu.Inatupasa kutumika kwa moyo na kujishusha
mbele za Mungu kwa kufuata maagizo na amri zake tuwaze mawazo mazuri ambayo
yatatufanya tuwe na Tabia nzuri na Mungu atapata nafasi ya kukaa kwetu kutokana
na mwenendo wetu mzuri .
Subscribe to:
Posts (Atom)