Na; Cyprian Sallu
Wapendwa katika maisha ya mwanadamu lazima kuwepo na mambo
mbalimbali ambayo yanaendana na maisha yake pamoja na mazingira ili kukamilisha
mfumo kamili wa maisha ya kiroho na kimwili.Hayo yote yaliyotajwa hapo yanaitwa TABIA.Tabia huleta picha kamilsi ya
mtu na mfumo wake wa maisha vilevile
hujulikana haraka sana kwa jamii inayozunguka eneo husika au mtu Fulani kwa
sababu wao ndio wanao kuona siku zote.Mara nyingi tumekwepa sana kutazama tabia
zetu na tukajishughulisha sana na mambo ya kanisa jambo ambalo husababisha
kutokea kwa dhambi.Lakini Tabia ya mtu si rahisi kubadilika mpaka Mungu mwenyewe ambadilishe na
amshuhudie kuhusu tabia yake.
Mtume Paulo alipewa neema na Mungu katika kujua tabia ya
wakristo huko Effeso na Korintho alibahatika kufahamu tabia na mwenendo wa wakristo katka kila kanisa kupitia njia ya roho,mafunuo .na shuhuda ndio
maana alisema, ‘’Sikuweza kusema nanyi kama watu wenye tabia ya rohoni bali kama watu wenye
tabia ya mwilini kama watoto wachanga
katika kristo’’.Alieleza hivyo kwa mtazamo wa tabia zetu sisi wanadamu na
maisha yetu kwasababu lazima kila mtu aishi chini ya mwongozo wa neno la mungu ili kwamba Tabia zetu ziwe za kiroho
na kuwa Baraka kwa wenzetu sio vikwazo.
Kutokana na hayo tabia ikajigawa katika makundi mawili TABIA NZURI NA TABIA MBAYA .Lakini pia katika hayo makundi mawili yanajumuisha aina zifuatazo za
Tabia katika maisha ya Mwanadamu ambazo zinahitaji utashi katika kufanya
uamuzi na kuishi kwa kuepuka vikwazo nza mitego ya shetani.
Aina za Tabia:
01.Tabia ya Kurithi:
Aina hii ya Tabia ni
vigumu kuifahamu na kuitambua endapo hutakuwa mfuatiliaji na usipo vunja laana
za ukoo maana hutokana na kurithi aidha kwa kupitia majina ya kurithi kutoka
kwa vizazi vyetu.Katika kurithi kunaweza kuwa na Tabia nzuri au Tabia mbaya ,
hivyo basi ni vizuri kila mzazi kuwa makini na kufuatilia kuhusu majina na vitu
ambavyo wanarithisha watoto wao.Mfano
wa tabia ambazo zinaweza kurithiwa,Uchawi,Uongo,Kiburi,Hasira na Nyingine
nyingi.
Umakini unahitajika katika kuepuka aina hii ya Tabia
kwasababu jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kurithishana hasa majina Mfano, Mtoto anaweza kuzaliwa akapewa jina
la babu yake lakini wazazi bila kufahamu
na kufuatilia historia ya mwenye jina wajikuta wamempa mtoto jina bila kuvunja
laana na kulitakasa jina lhilo upya ili mtoto asiweze kurithi hizo tabia za babu yake.Ni jambo gumu sana kwa mtu
asiyeamini na kufuatilia maandiko ya neno la mungu kwasababu laana imezungumzwa
katika biblia kuwa inaweza kumktesa mtu bila yeye mwenyewe kujua,unaweza kuona
mtu hafanikiwi au kila akifanya jambo haliendi vizuri anakimbilia kwa waganga
wa kienyeji akienda kusafisha nyota kumbe siri imejificha kwenye laana ya
kurithi jina la mtu wa zamani .Hivyo basi ni
vema kila mmoja kufuatilia asili ya jina lake na historia ya ukoo wake
ili kuepuka kuwepo kwa tabia za kurithi bila yakujua.
02.Tabia ya Kuiga
Tabia hii inakundi kubwa la watu wambao wameathiriwa
kwasababu ya mabadiliko ya mfumo wa maisha na utandawazi hasa vijana ambao hupenda sana kuiga Tabia ,mienendo na mifumo
ya maisha bila kufahamu hapo baadaye.Mara nyingi watu huiga kutoka kwa
marafiki,ndugu na jamaa kwa lengo la kuwaridhisha au kujiridhisha wenyewe
kwamba wanaenda na wakati lakini hawajui nini madhara ya kuiga.
1 Waebrania 13;17,
anatufundisha Tabia zitupasazo kuwa nazo kuwa tuwa tii wale wanaotuongoza tena
tuwaige na kufuata mienendo yao mizuri na ndio maana wakristo wengi wanabatizwa
majina ya watakatifu waliopita Mfano , Petro,Musa,Paulo,Mathayo na wengine
wengi.Vijana wengi wameingia katika kundi
hili la kuiga ilikuonekana wakotofauti na wengine lakini sababu kubwa ni
kutokulifahamu neno lamungu pamoja na historia ya ujana wa Yesu,hivi leo kijana
anaeokoka huonekana mshamba lakini
kijana aliyejiingiza kwenye kuiga mambo ya kigeni kama vikundi vya wacheza
disco,walevi na wahuni anaonekana wa maana kuliko Yule aliyeko kanisani.Ni
wakati wa kila kijana kujitambua na kijijengea tabia nzuri yenye misingi na
misimamo ya kiroho ili kujiwekea heshima kwenye jamii na maisha yake ya kiroho
yakiwa ushuhuda kwa kuutumia ujan wake vizuri bila kuiga mambo yasiyo na maana
mbele za Mungu .
Hata jamii nzima ya kitanzania imeanza kuiga utamaduni mbovu
kama ndoa za jinsia moja ambazo hazipo kwenye neno la Mungu na ni tabia ya
kishetani. Ni jukumu la watumishi wa Mungu
na wazazi kuwajengea watoto na kurekebisha tabia ya kuiga ,pia kuna baadhii ya
watumish nao wanaiga mambo jambo ambalo linahuzunisha na linapoteza heshima yao
katika utendaji wao kwasababu hakuna Nabii wala Mtume mwenye historia ya tabia
hii ya kuiga. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kujitengenezea na kufuata tabia za
kiutauwa na kuenenda akiwa ongozwa na
roho mtakatifu ili kuepuka kuiga mambo yasiyoendana na ukristo pamoja na
maagizo ya Mungu wetu vile vile ni heri kuiga mambo mazuri kuliko mabaya
03:Tabia Ya
Kuambukizwa:
Hii ni Tabia ya mwilini,katika amri zote mwanadamu anatakiwa
ajihadhari na mawasiliano ya mtu yeyoytekidamu ndio maana imeandikwa dhambi zote tunazofanya
ni makosa lakini dhambi ya uzinzi na uasherate ni dhambi ya damu
kuna kuambukizana tabia kuna kuambukiza hali mbaya .Enzi hizo wayahudi wakikuta
mtu anazini lazima apigwe mawe afe maana wamekwisha kuambukizana uzinzi natolea
mfano uzinzi na uasherati kwasababu ni dhambi ambazo zinaambukizwa kwa
kushawishiwa mtu hawezi kufanya akiwa
peke yake na zipo Tabia nyingi za kuambukizwa hivyo ni jukumu mkristo kutambua .
Ukahaba ni mmoja wapo ya tabia ya kuambukizwa |
Madhara ya tabia hii inaweza kukufanya ubaki pale pale
kimaendeleo unapoambukizwa dhambi au tabia yoyote ambayo sio nzuri ni vigumu
kutoweka katika mfumo wako wa maisha ,mara nyingi epuka kujichanganya kwenye
makundi ambayo hayana tabia kama yako kwasababu kinga ni bora kuliko tiba
hivyo jikinge juu ya watu wenye uwezekano wa kukuambukiza tabia mbaya . Hizo
ni baadhi ya Tabia za wanadamu tulio wengi ambao wakati mwingine tunaifanya
mioyo yetu kuwa migumu kwa kutokuiga mwenendo wa mungu aliyetuumba na kuacha
kuzifuata amri zake.Wakati mwingine tuna chelewa kupokea ahadi za mungu
kutokana na Tabia zetu kutokumpendeza yeye katika 2
Petro2 neno linasema kwamba bwana
hachelewi kutimiza ahadi zake na anaiona Tabia yetu sisi lakini anatuvumilia na
kutufundisha kupitia neno lake kuwa kama tabia zetu sio njema tufanye toba ya
kweli kwani tukifa katika tabia mbaya tutaingia katika hukumu.Ni lazima kila
mmoja achuchumilie kuishi maisha ya utauwa wa mungu na kujitahidi kuondoa Tabia
za mwilini ambazo zimepelekea kwa wakristo wengi kuyumba katika huduma
walizoitiwa na mungu.
Ili uwe na tabia nzuri au njema lazima upambane vizuri juu
ya roho na mwili maana roho hushindana na mwili maana wakati mwingine roho inaamsha
tama au vitu na tabia ambazo mwili hauzitaki lakini mara nyingi wakristo
tumeshindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi na kufuata tama za mwili na kuwa
maajenti wa shetani bila kujua kutokana
na kuingiwa na roho chafu kwasababu ya Tabia zetu tulizo nazo.Shetani amekuwa
macho akitazama Tabia zetu hivyo akiona tabia yako mbovu anaingia kwa
urahisi vile vile jinsi tabia yako ilivyo kutakufanya uingie jehanamu au
uzimani.
Dawa Ya Tabia Mbaya:
Tabia mbaya inabadilishwa na Neno la Mungu likiingia ndani ya moyo wa mwanadamu linasafisha
na kuondoa roho ngeni na Tabia zake jambo
ambalo hutokea baada ya wewe mwenyewe kuamua kumpa Yesu maisha yako na
kukubali kuwa neno la Mungu ni dawa na suluhisho la shida zako.
Yesu ni dawa ya tabia mbaya ukiamini na kufuata neno lake... |
Wito Kwa Wote;Wakati wote tukumbuke mwanadamu aliumbwa na Mungu
hivyo ni lazima afanye na kufuata mapenzi na amri za mungu ili asimuudhi tena
tusiweke ushabiki katika kumtafuta mungu na ufalme wake lakini kwa wakati huu
Wainjilisti,Wachungaji Na Wanaojiita Manabii wamekuwa na Tabia ya kujitwalia utukufu
kwamba wao ndio wanamtuma Mungu na wanaponya wagonjwa, kutoa pepo kwa nguvu zao
jambo ambalo halileti picha nzuri kwa watu mnao waongoza pia kuibua kiburi cha
imani kati ya dhehebu na dhehebu.Inatupasa kutumika kwa moyo na kujishusha
mbele za Mungu kwa kufuata maagizo na amri zake tuwaze mawazo mazuri ambayo
yatatufanya tuwe na Tabia nzuri na Mungu atapata nafasi ya kukaa kwetu kutokana
na mwenendo wetu mzuri .
nime farijika sana sana na maelezo kupitia ukurasa huu Mungu awabariki mzidi kutupatia majibu ya maswali inayo umiza moyo na kutesa akili pasipo kujua wapi tupate ushauri na nini kufanya kuepuka dhambi
ReplyDeleteIf Jesus made light of our life nobody will restrict the stages we made
ReplyDelete