Tuesday, February 5, 2013

UBATILI MTUPU


 

Na Paul Nhwani.
             
Mhubiri  12:1-11
Mfalme Suleimani anashuhudia kuwa alikuwa na mali nyingi pamoja na hekima ,lakini licha na hayo  bado akayaona yote kuwa na ubatili mtupu.licha ya hayo suleimani akaona yote ni bule usipomcha Mungu.(Mhubiri 12:13),japo alilalamika sana lakini aligundua na kusema kuwa mwanadamu lazima umche Mungu na umuhofu  MUngu pia.Suleimani  baada ya kugundua kuwa ya duinia  yanapita akaona  kuwa ni Ubatili  ni vema kumjua Mungu.
         Kwa hiyo Mfalme Suleimani anatupa maana halisi ya Ubatili kuwa  ni  kitu kisichokuwa na thamani ya kweli au ya kudumu,sasa jiulize hicho unachosumbuka nacho  kitakufikisha kwa Mungu au ndio ubatili mtupu alioona Suleimani?Maisha yetu ni mjumuisho wa mambo matatu yanayo tuzunguka ambayo ni ;MAWAZO,MANENO,MATENDO,NA MWENENDO. Tunaweza tukashidwa kufikia hatma ya mafanikio ya kumwona Mungu kutokana na mawazo maneno na matendo yetu kwa wennzetu endapo hatuwatendei yaliyo mema.kutokana na wanadamu wengi kujipenda sisi wenyewe na kuthamini mambo yetu,na kusahau kuwa Mungu ameagiza  tupendane zaidi, hata Yule ambaye kwako amekuwa ni kwazo kwako mara nyingi unaagizwa kumpenda.
                  Mambo yafuatayo yanaweza kutufanya tusifikie hatima njema ya kumwona Mungu na kujikuta tukibaki kujiita walokole bila kujua nini hatima yetu hapo baadae katika maisha ya kiroho.

01; Mienendo yetu mbele za watu na Mungu.
  Mambo haya yanaweza kuwa ubatili na kutufanya tushidwekufikia hatma njema  ya kumwona Mungu.(Mathayo 6:1-2).Mahali pengine tunafanya vitu ili tusifiwe na kuangaliwa na watu.Ukifanya  hivyo jua utapata malipo na thawabu za watu sio mbele za Mungu ,kwa hiyo tuangalie mwenenendo na tabia zetu.

02.Wanadamu kuwa  wasikilizaji wa neno na sio watendaji.
Watu waliowengi wanasikia na kuandika sana mafundisho ya neno la Mungu lakini hawayatendei kazi.Neno la Mungu ni kioo cha rohoni ambalo linatuonesha jinsi tulivyo,kwa maana nyingine linatuonesha  maisha ya mahusiano yetu na Mungu.lakini tumekuwa tukiyakimbia makusudi ya neno la Mungu juu yetu.Katika( Yakobo1:22-27). Tunaoneshwa kitu kinachosababisha tushindwe ni kuwa wasikilizaji tu na sio watendaji hivyo ni vizuri kila anaesikia neno la Mungu  kulifanyia kazi
                                                                                                                                                                                         03;Kuwa watu wa kujihesabia  haki na kuwahukumu wengine.
  Mambo ya kuhukumu  na kujihesabia haki, huo ni ubatili  mbele za Mungu .Mwinjilisti Mathayo  anasema (Mathayo 7:1-5),neno la Mungu linasema kuwa hatuna  ruhusa ya kuhukumu,na ubaya wa ubatili unakufanya  ujione muda wote  kuwa uko salama .Suleimani  alikumbushwa na Mungu,lakini kama asingekumbushwa na Mungu  yamkini hata sisi tusingepata nafasi hii ya kuoywa.
                                                                                                                                                                                                                                     04.Kuishi maisha ya uchungu na hasira
 Licha ya kuwa  watu wengi  wanatendewa mambo makuu na Mungu ,bado ndani yao  wanauchungu  wa kutokuwasamehe  wale waliowakosea.Hii inasababisha watu wasizione Baraka za Mungu na kama tutadumu katika haya ya kutokusamehe hatuwezi kufikia hatima  njema ya kumwona Mungu .Paulo anasema( Efeso 4:31-32).kusamehe kunatakiwa  ukate shauri  la kumsamehe  mtesi wako,ili ufike hatma ya kumwona Mungu.
05.Kutokuwa  na furaha katika Bwana.
Watu wengi furaha yao iko kwenye vitu,mali na katika matokeo mazuri sana,ambayo wanatendewa  na Mungu na sio katika Kristo Yesu.Hivyo basi inatupasa  kujitahidi pasipo kujali kuwa ni mzima au ni mgojwa,umepata au hujapata,umefanikiwa au hujafanikiwa,jitahidi mda wote  furaha yako iwe kwa bwana.(Wafilipi 3:1).Tufurahi katIka Bwana  na sio katika vitu, hali au matokeo mazuri.

06.Kutokuwa na upendo.
Katika maandiko matakatifu tunaagizwa kuwapenda zaidi wale  ambao wako kinyume na sisi ,lakini tumeshidwa kusimama sehemu hii zaidi  tumewahukumu wengine na  kuwaona kuwa ni waovu.Fahamu  kuwa hii inaweza ikasababisha usifikie hatma njema,Kwa kuwa Mungu ambaye ndiye tunaemwamini  yeye mwenyewe  ni upendo na alitupenda sisi kwanza.(Mathayo 5:43-45) utapata ukamilifu kwa kuwapenda  wasiokupenda  ili upate thawabu kwa Mungu wako,kwa kutokufanya hivyo  maisha yetu yatakuwa ni ubatili mtupu
.
07.Kujifanya  kuwa tunampenda  Mungu  kumbe ni uongo.
Waliowengi wanajifanya wanampenda Mungu sana lakini wanayoyafanya ni mabaya,(Mathayo 15:7-9),angalia na chunguza sana maisha yako .Mtu anaye mpenda Mungu haoni  taabu kusoma neno lake, kutoa sadaka nzuri, na kuonesha upendo kwa wenzake.hata kuweza kujitoa kwa wale wasiojiweza,  wanaohitaji kama yatima wajane,pamoja na vikongwe ,tukifanya hivyo Mungu ataonekana kwetu na tutavuna Baraka.
Na hitimisho la haya yote  (Mhubiri 12:9) jichunguze ndani ya nafsi ni lipi linaloweza kusababisha ubatili  katika maisha yako na Mbele za Mungu wako.Makusudi ya Mungu kwa wanadamu ni matatu (3)  KUMJUA MUNGU,KUMPENDA,NA KUMTUMIKIA

5 comments:

  1. Brother Paulo,

    I do appreciate to have read your article while in Mbeya. It makes me feel like I'm still there watching you teaching us the word of God. I'm so happy and God bless you. Please keep it up.

    Emily Mtauka.

    ReplyDelete
  2. asante sana maana ili neno nimelifundisha leo tarehe 17,22023

    ReplyDelete
  3. Mungu akubariki na Mimi Leo tar 27/9/2023 nimepata kibali kusoma mafundisho haya baada ya miaka 10.nimejifunza kitu Cha kunivusha

    ReplyDelete