Friday, February 8, 2013

:SIRI ILIYOKO KATIKA MWILI,NAFSI NA ROHO

Na Mwinjilisti Reuben





                                                                                                                                                                                        Tumwombe Mungu atujalie kuyajua mapenzi yake ,tabia yake namna  mpangilio na mapenzi yake.Watu wengi wanajuhudi katika Mungu lakini hawana maarifa ya  kumjua Mungu, kwamba tukienda kwake twende kwa namna gani ,kwamba yeye anatujua , lakini anatuona vipi hapo ndipo kuna ugumu.tunafika wakati tunamwona Mungu hawezi na hatusaidii ,kawaida huwezi kumfahamu Mungu ikiwa wewe mwenyeewe hujifahamu.  
       Huwezi kumfahamu Mungu ikiwa wewe mwenyewe hujifahamu ulivyo mbele za Mungu,kwa kuwa Mungu anasema tusafishe kabisa nafsi zetu ,mwili na roho pia kwa maana hiyo tuna sehemu kuu tatu  ambazo mwanadamu anatambulikwa kwazo nazo ni mwil,nafsi na roho. katika mwili tunajitazama  kwenye kioo kuweza kugundua kasoro tulizo nazo,lakini katia nafsi tuna misisimko hisia pamoja na utashi,lakini  katika roho tunalo neno la Mungu ambalo ndicho kioo  kinachotufanya tujitazame jinsi tulivyo na tuweze kujifahamu kuwa ni wazinzi, waongo ,wafitini ,wambea.1Wathesalonike5:23”,Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa nanyi nafsizenu miili yenu  mhifadhiwe muwe kamili bila lawama wakati wa kuja kwake bwana wetu Yesu kristo”.
     Hivyo basi walio wengi wanajua kuwa wameumbwa katika sehemu hizi tatu  lakini hawajui kazi za Mwili,Nafsi na Roho na kama hujui kazi hizo  hilo ni tatizo kwa kuwa  mwili utauchafua roho na nafsi vitashidwa kupokea Baraka  na neema za Mungu.Na endapo ukizijua kazi hizi wakati neno la Mungu likija kwako utagundua kuwa neno hili limekuja kwaajili ya mwili nafsi au roho.1Wakoritho2:10-12.Upya unaosemwa katika biblia ni neno maana anasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona,inamaanisha tumeponyeshwa roho na nafsi na sio mwili,na kama Mungu ameshatupa inatakiwa sisi tupokee.

    Yapo Mambo Manne ambayo Unapaswa Uyafahamu.   

               Mwili unapingana na roho.wagalatia 5:17 katika maisha kuna vitu ambavyo mwili unavitaka na roho haitaki, roho inataka ila mwili hautaki,lakini ili uweze  kupata Baraka na neema za Mungu  ongozwa na neno na uifuate roho yako.Yohana6:63 .ukikubali neno la Mungu likuongoze  jua kuwa uzima wa Mungu unao, lakini ukiongozwa na mwili lazima utashidwa kwa kuwa mwili unatabia zake unania zake na na unamahitaji yake pia.tabia za mwili 1wakoritho3:1-3
-Ukiwa na tabia za mwili  huwezi kupata vitu vya rohoni,ni lazima ujichuje kuingiakatika tabia   za roho ili uweze kupokea Baraka Wagalatia5:24
,Mwili una nia yake mawazo yake,na maana ya nia ni mwelekeo wa kufikia hatma fulani kwa hiyo basi mwili kuna sehemu unataka kufika na roho pia kuna sehemu inataka kufika.Warumi8:6-8 ,nia ya mwili ni katika dhambi na nia ya roho ni  kuiona mbingu.Naomba uelewe kuwa mwili unatabia zake, kama vile ulevi uongo husuda, uzinzi na nyinginezo,na tabia za rohoni pia ni upendo, unyenyekevu,ukarimu pamoja na nyinginezo,na mtu anayeishi katika haya ana matumaini ya kufika mbinguni.
Unapokumbana na matatizo  mpaka ukahisi mifadhaiko ya kumkufuru Mungu ,jifunze  kwa waliopitia magumu na wakashinda kama vile Ayubu3:2-11.Watu wengi  tunapokumbana na wakati mgumu  ndipo tunapomwacha Mungu na kuangamia.jifunze kwa Daudi pia 1samweli30:1-4,6 Daudi alijitia nguvu  katika bwana akashinda,na wewe pia inatakiwa ujitie nguvu katika bwana.Wapendwa tuangalie jinsi ya kujitia nguvu katika bwana ili na sisi tuweze kushinda.
    
1.Tengeneza  mahusiano yako na Mungu.
     Unapokumbana na matatizo  ukawa mtu wa kulaumu ,jua unamchukiza Kristo  zaidi amini kuwa Mungu anakupenda sana zaidi ya unavyofikilia na anakuwazia mema wala siyo mabaya,hivyo jitahidi utengeneze mahusiano yako na Mungu.Warumi8:35,zab 107:19-20, waebrania4:12

2.Tafakari na kumbuka ahadi za Mungu.
      Mungu  alikuahidi nini  katika  neno lake,Kumb20:1 jua kuwa Mungu anasema na roho  wala haihusiani na milango ya  fahamu iliyo katika mwili ni tofauti kabisa.Yohana1:1…,11-12, kumb 8:18

3.Tengeneza picha  kuwa kile ulichoomba umeshapokea.
      Liamini neno la Mungu na uwe na imani ya yale uliyoomba  kuwa umeshayapokea.Warumi4:20, 10:17 jitahidi ukuze kiwango cha imani yako kiwe juu.

4.Jizoeshe kuisemesha nafsi yako.
     Jitahidi kuisemesha nafsi yako  aidha ni kuikanya au kuionya,kile ambacho Mungu anakituma kwako  kupitia neno lake hakikisha unakikubalisha katika nafsi na roho yako,elemea mwili wako  ili roho yako  iinuliwe.

5.Jenga tabia ya kufunga.
Jifunze kuwa na faragha na Mungu katika hali ya kujinyima katika mwili kwa kufunga,Kufunga kumegawanyika katika sehemu mbili,kunakufunga kuunyima mwili chakula,na pia mfungo wa aina ya pili ni kufunga nafsi yako, yaani kuinyima nafsi yako kuhitaji na kutamani vitu ambavyo mbele za Mugu ni vibovu.Na ukifunga kwa kusimama na neno la Mungu yeye ni mwema atatenda sawasawa na alivyoahidi.

 




No comments:

Post a Comment