Friday, February 8, 2013

IMANI YAKO IPO WAPI?

Na Mwinjilisti Reuben












Imani ni kuwa na hakika ya mambo ambayo hayajawa bado.Inatakiwa uione kazi,biashara na mafanikio ya maisha pasipo uhalisia kwa kufanya hivyo utakuwa umetimiza imani ya kufanikiwa hivyo utaishi maisha ya kumpendeza kwa  kutarajia yale uliyoyaamini kama atakutendea.Mungu amegawa imani kwa kila mtu pia anataka imani iendelee kukua ili uvune Baraka kwake.(Warumi 12:3),. (Waebrania 11;6) tunaelezwa kuwa Kitu ambacho kinampendeza Mungu ni Imani ,kwa maana hiyo pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu.                                                                                                                                                           Kazi za shetani ni  kuiba,kuchinja na kuharibu lakini Bwana Yesu alikuja tuwe na uzima kisha tuwe nao tele,shetani anatuibia,anachinja imani na kuharibu kwa kuwa anajua akifanya hivyo hautakuwa na nafasi ya kumwamini Mungu.Imani ni kuwa na hakika ya mambo ambayo hayajawa bado,inatakiwa uione kazi,biashara na mafanikio ya maisha pasipo uhalisia ,kwa kufanya hivyo utakuwa umetimiza imani ya kufanikiwa hivyo utaishi maisha ya kumpendeza kwa  kutarajia yale uliyoyaamini kama atakutendea.Mungu amegawa imani kwa kila mtu pia anataka imani iendelee kukua ili uvune Baraka kwake.(Warumi 12:3),.

Kuna aina nyingi za imani lakini hapa tutazungumzia aina tano,ambazo mara nyingi tunakutana nazo katika maisha yetu ya kiroho na kimwili
.
01.Imani Iliyosukumiwa mbali.
 Hii ni imani iliyo tupwa ,na kuna watu wengi wanaomuona  Mungu kupitia ishara na miujiza lakini bado hawamwamini kwa maana hiyo wanaitupa imani.Paulo anasema hawa wamekabidhiwa kwa shetani ,na shetani akiwa  kwako uliyekuwa unamjua Yesu halafu ukamkana hali yako inakuwa mbaya kuzidi uliyokuwa nayo mwanzo  kwa sababu hata weza kukutendea muujiza kwa kutokumwamini kuwa yeye anaweza.

02.Imani Iliyokufa.
Hii ni imani ambayo mtu anaamini kuwa Yesu yupo lakini hatendi mema ,imani pasipo matendo imekufa,neno linahubiliwa lakini kile kilichohubiliwa huendi kukitenda lakini kwa kawaida  imani iliyo hai il itimie  lazima ulichoelekezwa na neno la Mungu inatakiwa ukifanye.Neno la Mungu linatuagiza kuwa tusiogope kwa kuwa aliye ndani yetu ni mkuu zaidi kuliko vyote,hivyo ondoka katika imani iliyokufa.

03.Imani ya Kweli.
Hii ni imani ambayo haina unafiki  wowote wala uongo ndani yake,kwasababu imani yenye unafiki ni yakuigiza wala siyo ya kweli na kuna watu ambao wanayo.Wanahofu ya kibinadamu wala hawana hofu ya kimungu.Imani ya kweli inasifa hizi;
                ­­-Inamtazama Yesu
                -Inakiri haimwonei aibu Yesu.
                 -Inatuliza moyo haina jaziba
                                                                                                                                                                                                                                                                  
 04.Imani Haba.
Ni imani ndogo sana,hii inatilia shaka juu ya mahitaji ya mwili lakini neno la Mungu linasema  atatupa vyote kwa kuwa hata tukijisumbua hatuwezi kuongeza hata urefu wa kimo cha mkono wetu.ikitokea dhoruba inatoweka.(Mathayo 8:26) na wakati wa matatizo imani hii inadhihilika kwa sabababu inamezwa na matatizo.(Mathayo 14:30) Petro alikuwa na imani lakini alipoingiza mashaka ndani yake ndipo alipoanza kuzama,jitahidi shida na matatizo uliyonayo yasikuzidi uwezo maana yanaweza kukuzamisha .
 Pia imani hii inasahaulisha mambo makuu aliyokutendea Mungu(.Mathayo16:9-10) usiwe na imani haba unapokumbana na matatizo,tafakari ni yapi uliyovushwa kwa neema  ndipo ujitie nguvu usonge mbele.

05;Imani Kuu.
(Mathayo 8;8-10), Ukitangaziwa uponyaji aminikuwa umepona,hii ndio maana ya Imani Kuu ya kutegemea neno la Mungu na kulifanyia kazi ,zifuatazo ni sifa za Imani Kuu.
-Ukiing’ang’ania huwezi kumuacha Yesu( Mathayo 15 ;21-28).
Kuna watu wakiombewa wanakuwa wepesi wa kukata tama wakati wa kusubiri majibu ya maombi yao hivyo ni heri kuvumilia kwasababu Mungu antenda kwa wakati wake kwahiyo uwe na Imani kwa neno utakalosikia kutoka kwa watumishi wa Mungu.
     Ni wajibu na haki kwa kila mkristo anayemuamini Mungu kujihoji na kufahamu imani aliyonayo ni ipi na ipo kwenye kundi lipi,je ni Imani Haba,Imani iliyotupwa au Imani kuu, na kwakufanya hivyo kutatuweka katika nafasi nzuri kwenye mahusiano kati yetu wanadamu na mungu aliye mbinguni.

No comments:

Post a Comment